Wivu ni kitu kibaya na kwa tafsiri ya wivu hakuna wivu mzuri wala wivu mbaya. Wivu ni wivu tu. Hivyo basi, wivu ni kujiona wewe una stahili zaidi kuliko wengine. watu wenye wivu ni watu ambao hawana raha kabisa na maisha yao yaani wanapoona mwingine kafanya kitu roho inamuuma sana. wivu unawatafuna watu kiasi kwamba wanakuwa wanaishi maisha ya utumwa sana.

Muda tulionao

Rafiki,ukishakuwa na ile hali kwanini wengine wafanikiwe utaumia sana. ukiwa si mtu wa kupongeza pale wenzako  wanapofanya mazuri  ni dalili ya kukaribisha wivu kwenye maisha yako. wivu unazaa chuki kubwa katika maisha yetu na chuki inakuja kuzaa mauti. Kwahiyo, wivu unaua kwa lugha nyingine, natumaini umeshawahi kusikia watu wanajinyonga kwa sababu ya wivu na mambo mengine yanayohusiana na hayo.

SOMA; Huu Ndiyo Wakati Sahihi Wa Kutua Mizigo Tuliyobeba Kwenye Mioyo Yetu.

Kadiri ya st. Augustine mtu mwenye wivu hana upendo. Mtu yeyote ambaye ana wivu hana upendo kwanini? Kwanza upendo huwa haukasiriki pale unapomwona mtu mwingine akifanikiwa au unapomtendea mwingine mazuri. Upendo huvumilia yote na wala upendo hauhusudu. Hakuna kitu kama upendo hapa duniani kwanza tu tunavyoishi hapa duniani kila siku ni kwa ajili ya upendo kama siyo upendo hakuna maisha.

Ukiwa ni  mtu ambaye una wivu basi wewe huna upendo, utakuwa ni mnafiki. Watu wanaweza kujifanya wana upendo kwako kumbe wana upendo wa kinafiki yaani ule upendo wa machoni. Kuna ule upendo mwingine ambao mtu anakupenda kwa sababu ya kitu fulani yaani upendo wa vipimo.

mpendwa msomaji,” kipimo cha upendo ni kupenda bila kipimo”. Kama mtu akikuchukia bila sababu, anakuonea wivu tu wewe kaa chini na fanya kitu hiki kimoja nacho ni chunguza kiini cha kosa. Chugunza kiini cha kosa ndiyo, jiulize kwanini ananichukia bila sababu? Ukiona hakuna sababu basi mpuuzie endelea na maisha yako huo utakua ni wivu unaomtafuna. Mwekee kaa la moto kichwani na endelea na maisha yako mwache wivu uendelee kumtafuta kama umechunguza na hujaona sababu yoyote.

SOMA; Sehemu Ambayo Ina Idadi Kubwa Za Wafungwa Ukilinganisha Na Magereza Tunazozifahamu

Hatua ya kuchukua leo; acha wivu kwa sababu mtu ambaye ana wivu hana upendo. Ukisoma kitabu cha kwanini msamaha nimeelezea jinsi ya kukabiliana na wivu hivyo nakusihi rafiki kuwa mtu chanya na kuwa na upendo na watu wengine.

Mpendwa msomaji, tabia hasi kama vile wivu zitakupelekea kuyaona maisha ni machungu. Wivu ni kujibebea mizigo ya wengine na hivyo huwezi kuwa huru hata siku moja. Sasa kwanini uendelee na kubeba mizigo ya watu wakati ya kwako hujayamaliza? Huoni ni kupoteza muda na nguvu? Tua mzigo endelea na maisha yako huru.

Ukawe na siku bora sana rafiki.

Rafiki na mwalimu wako,

Deogratius Kessy

0717101505/0767101504

deokessy.dk@gmail.com , kessydeo@mtaalamu.net

Unaweza kutembelea tovuti yangu kwa kujifunza zaidi kila siku  ambayo ni www.mtaalamu.net/kessydeo .

Asante sana !