USHAURI; Jinsi Ya Kuzuia Changamoto Za Kifedha Zisizuie Mipango Yako Na Uwekezaji Wa Kufanya Unapokuwa Mbali Na Nyumbani.

Rafiki yangu mpendwa, Karibu tena kwenye makala yetu ya ushauri wa changamoto ambapo tunapeana hatua za kuchukua kulingana na changamoto mbalimbali ambazo tunapitia kwenye maisha yetu. Changamoto ni sehemu ya maisha, na hivyo dawa yake ni kuzitatua na siyo kukubali zituzuie au kuzitumia kama sababu ya kutokupiga hatua zaidi. Ukikubali changamoto ikuzuie maana yake unakuwa... Continue Reading →

USHAURI; Hivi Ndivyo Unavyoweza Kutengeneza Mafanikio Makubwa Kwenye Maisha Yako Kwa Kuanza Na Mtaji Mdogo Kabisa.

Rafiki yangu mpendwa, Watu wengi wanapenda kupiga hatua kwenye maisha yao, lakini ni wachache sana wanaopiga hatua hasa na kufanikiwa. Wengi hubaki na matamanio ya kufanikiwa lakini wasifanikiwe. Na sababu huwa ni visingizio ambavyo wengi wanavyo. Watu wengi wana visingizio vingi kwa nini hawafanikiwi au kupiga hatua. Wana kila sababu kwa nini watashindwa na hivyo... Continue Reading →

USHAURI; Jinsi Ya Kupata Wafanyakazi Wenye Uaminifu Na Juhudi Kwenye Biashara Yako.

Rafiki yangu mpendwa, Vipo vikwazo viwili vikubwa kwenye ukuaji wa biashara. Vikwazo hivyo ni fedha na rasilimali watu. Biashara nyingi zinashindwa kukua na hata nyingine kufa kwa sababu uwekezaji wa fedha haufanyiki kwenye biashara hizo. Pia pale ambapo kunakosekana rasilimali watu, biashara haiwezi kukua. Pamoja na umuhimu wa rasilimali watu kwenye ukuaji wa biashara, watu... Continue Reading →

USHAURI; Hatua Za Kuchukua Pale Unapohamishwa Kazi Na Kupelekwa Eneo Ambalo Wengi Wanalisema Vibaya.

Rafiki yangu mpendwa, Changamoto ni sehemu ya maisha yetu ya kila siku. Tunaweka mipango fulani lakini mambo ambayo hatukuwa tumeyategemea yanatokea. Ni katika nyakati za aina hiyo wengi hukata tamaa na kuona hawawezi tena kupata kile wanachotaka. Na hapo ndipo wengi wanapokosea, kwa sababu hakuna changamoto ambayo ni ngumu na haiwezekani kabisa. Kila changamoto tunayokutana... Continue Reading →

USHAURI; Hatua Za Kuchukua Pale Wateja Wanapokuacha Na Kwenda Kwa Wafanyabiashara Wengine.

Rafiki yangu mpendwa, Karibu kwenye makala ya ushauri wa changamoto ambapo tunapeana hatua za kuchukua ili kuweza kuvuka changamoto zozote ambazo zinatuzuia kupiga hatua kwenye maisha yetu. Kwenye makala ya leo, tunakwenda kujifunza hatua za kuchukua pale wateja wanapokuacha na kwenda kwa wafanyabiashara wengine. Wote tunajua kwamba bila ya wateja, hakuna biashara. Hivyo jukumu muhimu... Continue Reading →

USHAURI; Njia Tatu Za Kuweza Kukuza Biashara Yako Pale Unapokuwa Na Changamoto Ya Kupata Bidhaa Bora Kwa Bei Nafuu.

Rafiki yangu mpendwa, Changamoto kwenye maisha ni mrejesho kwetu kwamba kuna kitu hatukifanyi vizuri au kuna kitu hatujajua bado. Hivyo badala ya kuogopa na kukimbia changamoto, tunapaswa kuzipanda na kuzikaribisha. Kila unapokutana kwenye changamoto kwenye maisha yako jiulize maswali haya mawili. Swali la kwanza ni kipi ambacho sijui kuhusu hili. Na swali la pili ni... Continue Reading →

USHAURI; Hivi Ndivyo Unavyoweza Kujua Biashara Ya Mtandao Iliyo Sahihi Na Kuepuka Kutapeliwa.

Rafiki yangu mpendwa, Karibu kwenye makala ya ushauri wa changamoto mbalimbali zinazotuzuia kufanikiwa. Kama ambavyo nimekuwa nakuambia mara kwa mara, usiombe kutokukutana na changamoto, bali omba kuwa imara ili uweze kukabiliana na kila aina ya changamoto. Kwa sababu changamoto hazitaisha, ila kadiri unavyokuwa imara ndivyo unavyoweza kuzikabili na kushinda. Kwenye makala ya leo nakwenda kukushauri... Continue Reading →

USHAURI; Jinsi Ya Kudhibiti Mzunguko Wako Wa Fedha, Kuituliza Fedha Mfukoni Na Kuongeza Faida Kwenye Biashara.

Rafiki yangu mpendwa, Kama walivyosema wahenga, fedha ni sabuni ya roho, fedha ndiyo kitu pekee ambacho kila mtu anakipenda na kina matumizi mazuri kwake. Vitu vingine vyote kila mtu ana upendeleo binafsi. Mfano kuna watu wanakula nyama na kuna ambao hawali nyama. Kuna wanaokunywa pombe na kuna wasiokunywa pombe. Lakini fedha, fedha ni nzuri kwa... Continue Reading →

USHAURI; Kwa Nini Kila Ukianzisha Biashara Inakufa, Na Hatua Za Kuchukua Ili Kufanikiwa Kwenye Biashara.

Rafiki yangu mpendwa, Karibu tena kwenye makala za ushauri wa changamoto mbalimbali tunazokutana nazo kwenye maisha yetu, ambazo zinatuzuia kufika pale tunakotaka kufika na maisha yetu. Changamoto siyo kitu kibaya, bali ni kiashiria kwamba tumejaribu mambo makubwa, mambo ambayo hatujayazoea huko nyuma. Hivyo kama tukitumia changamoto tunazokutana nazo kama darasa, tutaweza kupiga hatua zaidi. Kinachowaponza... Continue Reading →

Create a website or blog at WordPress.com

Up ↑